Hiyo
ilikuwa tarehe 30th September 2015, tarehe ambayo iliingia kwenye
historia kwa kila shabiki wa klabu na Ronaldo mwenyewe ambaye michuano
hii imekuwa uwanja wake mzuri wa kuongeza idadi ya magoli hasa msimu
huu. Kitu cha kushangaza Nahodha huyu wa Ureno, sio miongoni mwa
wafungaji bora watatu wa La Liga – yupo nafasi ya nne, magoli manne
nyuma ya Neymar, lakini hata hivyo Ronaldo anafanya vyema ulaya, mpaka
ameshafunika Lewandowski na Müller (Bayern), Dyzuba (Zenit) pamoja na
Luis Suárez (Barcelona).Leo usiku Cristiano Ronaldo pia atakutana na sura anazozifahamu – golikipa wa Malmo Johan Wiland ameshakuwa mhanga wa kasi ya ufungaji wa Ronaldo, na sio tu kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Swedbank Stadion. Katika msimu wa 2013/14, mreno huyo na golikipa wa kiswedish walikutana wakati Real Madrid walipocheza na timu ya FC Copenhagen katika hatua ya makundi.
Cristiano
alifunga mara mbili katika mechi ya kwanza ndani ya s Bernabéu na
akafunga goli lingine katika mchezo wa marejeano uliofanyika
Copenhagen’s Parken Stadion. Magoli hayo matatu na mawili aliyofunga
dhidi ya Malmo, yanafanya rekodi yake dhidi ya golikipa huyo wa
kiswedeni kuwa magoli matano.
No comments:
Post a Comment