Tuesday, 8 December 2015

MAN UNITED YAPIGWA, YATUPWA EUROPA,matokeo haya hapa nimekuwekea


8, 12, 2015
Image result for sign of uefa

UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mechi za Mwisho za Makundi
Matokeo:
Jumanne Desemba 8
KUNDI A
Paris St Germain 2 Shakhtar Donetsk 0           
Real Madrid 8 Malmö FF 0          
KUNDI B
PSV 2 CSKA 1                  
VfL Wolfsburg 3 Man United 2              
KUNDI C
Benfica 1 Atletico Madrid 2         
Galatasaray 1 FC Astana 1          
KUNDI D
Man City 4 Borussia Mönchengladbach 2         
Sevilla 1 Juventus 0         

Manchester United imefungwa 3-2 na Wolfsburg Bao 3-2 kwenye Mechi ya Kundi B la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL na kutupwa nje na sasa kucheza Raundi ya Mtoano ya EUROPA LIGI.
Kipigo hicho, na ushindi wa PSV Eindhoven wa Bao 2-1 dhidi ya CSKA Moscow, kumezifanya Wolfsburg na PSV kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya UCL na Man united kumaliza Nafasi ya 3.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Wolfsburg kucheza Raundi ya Mtoano ya UCL.
Huko Santiago Bernabeu, Cristiano Ronaldo alifunga Bao 4, Karim Benzema kupiga 3 na moja la Mateo Kovacic na kuwapa ushindi Real wa Bao 8-0 toka Kundi A.
Real, na PSG, ambao wameshinda 2-0 walipocheza na Shakhtar Donetsk zote zimesonga na Shakhtar itakwenda EUROPA LIGI.
Man City, ambao walikuwa washafuzu toka Kundi D, Leo wameichapa Borussia Mönchengladbach 4-2 na kumaliza kileleni mwa Kundi hilo na kufuatiwa na Juventus ambao Leo walifungwa 1-0 na Sevilla ambao wamemaliza Nafasi ya 3 na hivyo kwenda EUROPA LIGI.







No comments:

Post a Comment