Wednesday, 2 December 2015

KIBADENI ALIA NA CECAFA, ATOA UFAFANUZI WA MAGURI, BARTHEZ KUKAA BENCHI VS ETHIOPIA

Image result for kibadeni
 
 
 Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Abdallah Kibadeni amesema Ethiopia haikuwa na uwezo wa kukifunga kikosi chake, lakini walibebwa na Cecafa.
Kibadeni amesema Cecafa ilionyesha wazi ilitaka kuona Ethiopia wanafika mbali licha ya kuwa na kikosi kibovu.
Pamoja na hivyo, Kibadeni amesema hakuwampanga mshambuliaji Elius Maguri katika mechi ya pili ya Ethiopia hatua ya robo fainali kwa kuwa alikuwa na kadi mbili.
“Maguri na Aishi Manula walikuwa na kadi mbili za njano, lakini Barthez (Ally Mustapha) alikuwa mgonjwa,” alisema Kiabadeni.
Stars ilimaliza mechi zote mbili dhidi ya Ethiopia kwa sare ya 1-1 lakini hatua ya robo fainali ikatolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3.

No comments:

Post a Comment