MABINGWA
wa Germany na Vinara wa Bundesliga Bayern Munich Leo wameonja kichapo
chao cha kwanza kwenye Ligi ya Germany Msimu huu kwa kupigwa Bao 3-1
Ugenini na Borussia Monchengladbach.Hii ni mara ya pili tu kwa Bayern kupoteza Mechi Msimu huu baada ya kufungwa 2-0 na Arsenal Mwezi Oktoba kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Emirates.
Bao zote za ushindi wa Borussia Monchengladbach zilifungwa Kipindi cha Pili na Oscar Wendt, Lars Stindl na Fabian Johnson katika Dakika za 54, 66 na 68 na lile la Bayern kufungwa Dakika ya 81 na Franck Ribery ambae hilo ni Bao lake la kwanza baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 9 akiwa majeruhi.
Ushindi wao wa Leo umewaweka Borussia Monchengladbach Nafasi ya 3 wakiwa Pointi … nyuma ya Borussia Dortmund ambao Leo wameshinda Ugenini kwa kuifunga VfL Wolfsburg 2-1 na kujiweka Pointi 5 nyuma ya Vinara Bayern baada ya Mechi 15 kwa kila Timu.
Bao za Dortmund zilifungwa na Marco Reus na Shinji Kagawa wakati lile la Wolfsburg lilikuwa ni Penati ya Ricardo Rodriguez.
Wolfsburg walisawazisha Dakika ya 90 kwa Penati hiyo ya Rodriguez lakini Shinji Kagawa, alieingizwa Kipindi cha Pili, aliwapa ushindi katika Dakika ya 93.
Matokeo
Jumamosi Desemba 5
Hamburger SV 1 FSV Mainz 3
Hertha Berlin 2 Bayer 04 Leverkusen 1
Borussia Monchengladbach 3 Bayern Munich 1
FC Koln 0 FC Augsburg 1
FC Ingolstadt 1 TSG Hoffenheim 1
VfL Wolfsburb 1 BV Borussia Dortmund 2
No comments:
Post a Comment