![]() |
| Papa Francis amekuwa akihimiza sana kuhusu amani na maridhiano |
"Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la jini kupanda woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
"Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguze nyoyo za wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu."
Bofya hapa kwa habari za moja kwa moja kuhusu ziara ya Papa Francis
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa makanisa mengine akiwemo kiongozi wa Kanisa la Kiangilikana Kenya Dkt Eliud Wabukala.
Viongozi wa dini ya Kiislamu Kenya pia wamehudhuria mkutano huo, wakiongozwa na Prof Abdulghaful El-Busaidy.
Papa Francis amesema amekuwa akihakikisha kila aendako anatangamana na watu wa dini na imani nyingine.
![]() |
| Baada ya misa, waumini waliendelea kupokea komunyo |
“Afya ya jamii yoyote hutegemea afya ya familia. Kwa ajili yake, na kwa ajili ya jamii, Imani yetu katika neno la Mungu inatuita tuunge mkono familia katika jamii, kuwakubali watoto kama Baraka kwa ulimwengu, na kutetea hadhi ya kila mtu, kwa ndugu zetu wote katika familia moja ya binadamu,” amesema.

Watu waliohudhuria ibada hiyo walianza kuingia uwanjani mapema na walivumilia mvua ambayo ilianza kunyesha mapema asubuhi.


No comments:
Post a Comment