![]() |
STEVEN WASIRA |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jumanne tar 27.october 2015 majira ya jioni, Wasira
alisema matokeo ya ubunge yalichakachuliwa kutokana na uhesabuji kura
kutofuata utaratibu.
Wasira alisema kutokana na hilo, msimamo wake ni kutoyatambua
matokeo hayo yaliyomshangaza na kumwangusha katika mbio hizo za
kulitetea jimbo hilo.
Alisema kura katika uchaguzi huo ziliibwa na kilichotangazwa hakitokani na uamuzi wa wapigakura wa jimbo hilo.
Wasira alitolea mfano wa kituo kimoja cha kupigia kura, akisema kura 1,000 ziliongezwa kwa lengo la kumsaidia mpinzani wake.
Alifafanua kuwa kituo hicho cha kupigia kura kilionyesha kilikuwa
na wapigakura waliojiandikisha 367, waliopiga kura 276, kura halali
zilikuwa 271.
Lakini alisema matokeo katika kituo hicho yalionyesha kuwa chama
cha ACT- Wazalendo kilipata kura moja, CCM kura 120 na Chadema kura 749,
na Msimamizi wa Uchaguzi akatangaza waliojiandikisha walikuwa 1,367.
Alisema hatasaini matokeo hayo kwa sababu ni batili na hawezi
kuafikiana nayo wala kuyatambua huku akisisitiza uchaguzi huo
haukufanyika kwa haki. Hata hivyo, Wasira alisema Msimamizi wa Uchaguzi
wa jimbo hilo, Msoffe hakutilia maanani barua ya malalamiko aliyoandika
kupitia kwa Mwanasheria wake ili kusitishwa utangazaji wa matokeo hayo.
Hata hivyo, alikanusha tuhuma za kukimbilia jijini Mwanza kwa kile
kilichodaiwa ni kukwepa aibu ya kushindwa, bali alikwenda huko kwa lengo
la kupata ushauri wa nini cha kufanya katika kipindi hiki.
No comments:
Post a Comment