Monday, 26 October 2015

CAPITAL ONE CUP: JUMANNE MABINGWA CHELSEA UGENINI, ARSENAL WAGENI WA SHEFFIELD, JUMATANO MAN UNITED NYUMBANI NA BORO!


CAPITALONECUP-CHELSEA2015Mechi za Raundi ya 4 ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, zitachezwa Jumanne na Jumatano kwa Mechi 4 kila Siku,

Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Chelsea, Jumanne wapo Ugenini kucheza na wenzao wa Ligi Kuu England, Stoke City na Siku hiyo pia Arsenal watakuwa Wageni wa Timu ya Daraja la chini, Sheffield Wednesday

Jumatano, Manchester United wapo Nyumbani kwao Old Trafford kucheza na Middlesbrough wakati Man City nao wako Nyumbani kucheza na Crystal Palace.
Liverpool watakuwa kwao Anfield kuivaa Bournemouth.


Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku ispokuwa inapotajwa
Jumanne Oktoba 27

Everton v Norwich City
Hull City v Leicester City
Sheffield Wednesday v Arsenal
Stoke City v Chelsea

JUMA TANO 28

Liverpool v Bournemouth
Manchester City v Crystal Palace
Southampton v Aston Villa
2300 Manchester United v Middlesbrough

No comments:

Post a Comment