Siku ya kwanza ya mwezi September 2016 imekua ikitajwa sana kwenye headlines siku za karibuni na ni baada ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano nchi nzima, maandamano ambayo hata hivyo vyombo vya dola viliyapiga marufuku.
Leo August
31 2016 mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha
mikutano na maandamano kwa muda wa mwezi ili kuwapa nafasi wadau
mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kutafuta suluhu ya jambo hili kwa
kukutana na Rais na Serikali yake, Mbowe amesema…..
>>>’Sisi
tunawaheshimu viongozi wetu wa kidini tumekutana nao na kusikiliza wito
wao wa kuahirisha UKUTA kwa wiki mbili au tatu ili wapate fursa ya
kuzungumza na Rais Magufuli na Serikali yake, huu ni wito wa busara na
wenye kulijali taifa letu na wajibu wake sio wito unaopaswa kupingwa kwa
sababu nyepesi nyepesi’
No comments:
Post a Comment