“Sikuwahi kufahamu lolote la maana kuhusu soka kabla sijakutana na Johan Cruyff,” Guardiola aliwahi kukaririwa. Guardiola alikuwa kiungo katika moja ya timu bora za klabu ya Barcelona chini ya Cruyff. Cruyff sio tu kwamba alibadili mawazo ya kisoka kichwani kwa Pep, lakini mawazo yake juu ya namna ya kupiga pasi ndani ya uwanja na namna ambayo wachezaji wanatakiwa wakae uwanjani yalifanya mapinduzi kwenye soka.
Wengi wanaweza kuwa hawana kumbukumbu juu ya namna ipi Cruyff anaweza kuwa alichangia mawazo haya ya Pep juu ya namna golikipa anatakiwa kuwa ndani ya uwanja. Mwaka 1974, Cruyff alimsukuma kocha wa Uholanzi Rinus Michels kumchagua kipa Jan Jongbloed mbele ya kipa aliyeamikika kuwa bora Jan van Beveren kwenye kombe la dunia la mwaka huo. Huu ni mfano wa awali wa ubora wa mawazo yake.
Cruyff aliamini kuwa kipa anatakiwa kuwa bora sana kwenye ugawanyaji wa mipira kuliko hata kwenye uzuiaji michomo langoni. Alivyoanza maisha ya ukocha akiwa Ajax, Cruyff akaonyesha kuendelea kung’ang’ania filisofia yake kwa kumpandisha kipa Stanley Menzo kutokana na kuwa bora katika hili. Pia akamchagua kocha wa makipa kwa ajili ya kumlea Menzo aliyefahamika kama Frans Hoek.
Kuanzia siku hiyo, Hoek amefanikiwa kuwa mmoja wa wa makocha bora wa makipa kufikia hatua ya kufanya kazi na vilabu vikubwa kama Barcelona na Manchester United, huku akifanya kazi mara nyingi na Louis van Gaal. Kwa wengi huyu ni zaidi ya kuwa kocha, kwani alifanikiwa kuandika kitabu juu ya namna kipa anatakiwa kuwa. Mbinu nyingi Hoek amezitoa kwa Cruyff.
Hoek alichanganua kuna aina mbili za makipa ambao ni aina R (R-type) na aina A (A-type). Wa kwanza anafanya kazi kutokana na matukio yanayoendelea langoni (reacting to situation) na mwingine anaangazia ama kusoma mchezo unavyoweza kuwa (anticipates). Kwake anaamini makipa wote wapo kwenye hivi viwili. Pamoja na kuwa makipa wanaofanya kazi kutokana matukio (wachomoaji michomo) kusifika zaidi, yeye (Hoek) haamini katika hilo.
Edwin van der Sar aliwahi kumpongeza kama kocha aliyesababisha kuwe na uhusiano kati ya golikipa, mabeki na vungo”, na kuanzia kwa Jongbloed mpaka kwa Menzo, Hoek anapendelea makipa wanaojua kusoma mchezo yaani wale wenye tabia kama za wachezaji wa ndani. Pale Barca, wenye kumbukumbu mtakumbuka Vitor Baia alimpisha Ruud Hesp kwa sababu hakuwa huru kuwa mchezaji wa awali wa kuanzisha namna timu inatakiwa kucheza.
Mmoja kati ya watu ambao walikumbwa na akili hii ya Hoek alikuwa ni koacha ambaye alikuwa anaishi na kufanya kazi umbali wa kilomita 12,000 yaani kule Santiago, Chile. Huyu ni Julio Rodriguez ambaye alikuwa ni moja ya makipa bora kwa aina yake huku akisifika pia kuwa kuwa muokoaji mzuri wa penati.
Kwenye miaka ya 1990 alikuwa akifanya kazi kama kocha wa makipa kwenye klabu yake ya zamani iliyofahamika kama Colo-Colo, huku akijiendeleza katika taaluma hiyo kwa maana ya kuongeza elimu. “Nilikutana na Frans Hoek mwaka 1996,” Rodriguez aliwahi kuiambia Sky Sports. “Alikuwa akifanya kazi na Ajax pamoja na Louis van Gaal huku nami nilikuwa mkufunzi wa makipa vijana wa Colo-Colo kipindi hicho.
“Nilifahamu mengi kuhusiana na Frans kwa sababu aliwahi kutoa matoleo yanayofuatana matatu ya video juu ya suala la ukipa. Bado ni matoleo bora sana hata hivyo.” Yalikuwa mazuri kiasi cha kumfanya Rodriguez kusafiri mpaka Marekani kutaka kumwona, Hoek alivyogundua kuwa Ajax walikuwa Marekani. “Nilienda Marekani kumwona nikitokea Chile,” alisema Rodriguez.
“Nilipokutna naye kweye kliniki yao alinieleza kuwa kama nilipenda mafunzo na mawazo yake basi niende uholanzi nikapate kozi zake, na ndilo jambo nililofanya. Kwake makipa wanatakiwa kuwa kama wachezaji wa nafasi nyingine. Wanatakiwa kuwa wabunifu, wenye kuweza kutuliza mpira vyema na kuuongoza, kuweza kupiga pasi kwa usahihi sana na vyema, kupiga mpira kiuweledi, kucheza kama beki wa mwisho, na baada ya hapo kuokoa michomo”
Mawazo waliyojadili yalikuwa na tija sana kwa vilabu vingi maarufu nchini Chile, lakini hii safari ya Rodriguez’s trip proved particularly significant for one hopeful.inaweza kuwa ilikuwa na msaada mmoja kwa mtu moja mahsusi. “Nilijifunza kutoka kwake namna ya kutengeneza kipa wa kisasa,” aliongeza. “na siku zote nasema bila msaada wa Frans isingewezekana kuwa na mazao kama huyu Claudio Bravo.”
Katika majira ya joto ya mwaka 1996, Bravo alikuwa na umri wamiaka 13 tu na katika klabu ya Colo-Colo walikuwa wana wasiwasi kama angeweza kuja kuwa kipa mzuri hasa mwenye nguvu na muonekano wa kigolikipa. Bahati nzrui kuanzia hapo Rodriguez hakuwa miongoni mwao. “Alikuwa mwembamba sana na mfupi lakini mcheshi,” Rodriguez anasema. “Alikuwa mwenye tabia njema na ambaye siku zote angetaka kujifunza”
Bravo, kijana kutoka nje ya mji wa Santiago katika jimbo la Maipa alitengenezwa kuja kuwa aina tofauti kabisa ya golikipa yaani yule aina A (A-type) kwenye ule mfumo wa Hoek wa kuchanganua aina za makipa. Claudio Herrera ni mchambuzi wa soka kwenye El Mercurio, gazeti la nchini Chile na anasema Bravo alitwaa namba yake pale nafasi ilipowadia.
Jose Mari Bakero ambaye pia alikuwa kikosini pamoja na Guardiola kwenye eneo la kiungo kwenye kikosi cha Barcelona ya Cruyff, ndiye aliyemsajili Bravo kwenye klabu ya Real Sociedad. Alipendezwa na uwezo wake wa kutulia na mpira lakini bahati mbaya alifukuzwa katika msimu wa kwanza wa Brav kutokana na matokeo mabovu. Bravo aliwekwa benchi na kocha aliyefuatia ambaye ni Chris Coleman ambaye alimpenda Asier Riesgo.
Lakini pia kuna huyu mtu anayeitwa Lillo ambaye Guardiola alimpenda sana na alipenda aina yake ya ufundishaji kiasi cha kuamua kucheza chini yake kipindi cha mwisho cha maisha ya soka. Lillo alivyopewa ukocha wa Sociedad mwaka 2008 alimrejesha Bravo kikosini.
Ni huyu Lillo pia ambaye alikuwa msaidizi wa Sampaoli wakati Chile inatwaa ubingwa wa Copa America na Sampaoli anamwita mwenye akili nyingi. Huu wote ni mzunguko wa mikono aliyopita Bravo mpaka kwa Luis Enrique kocha wa Barcelona ambaye pia aliwahi kucheza na Pep na anayevutiwa na aina yake ya ukipa.
Hakuna namn ambayo ungeweza kupinga Guardiola kumchukua kipa huyu. Ana kila kitu anachokitaka na amepita katika mikono ambayo inaishi fikra zake, watu ambao wanaishi na kuamini kama yeye. Hii ndio sababu Joe Hart hawezi kuwa kipa wa Guardiola pamoja na kuwa muokoaji mzuri wa michomo kuliko makipa wengi duniani.
Makala hii kwa msaada wa Adam Bate, mchambuzi SkySports.
Nifuate Instagram @nicasiusagwanda
No comments:
Post a Comment