Droo ya raundi ya tatu ya Kombe la EFL (EFL Cup), kombe ambalo kwa miaka takribani minne nyuma lilikuwa likiitwa Capital One Cup kufuatia udhamini wa Capital One, imefanyika imefanyika jana baada ya raundi ya pili kukamilika rasmi.
Katika droo hiyo, vigogo Manchester United watakuwa ugenini kucheza na Northampton Town katika dimba la Sixfields Stadium.
Liverpool watasafiri kuwafuata Derby County baada ya kutoa kipigo kitakatifu cha mabao 5-0 dhidi ya Burton Albion kwenye raundi ya pili.
Leicester wakiwa nyumbani King Power Stadium watawakaribisha Chelsea, likiwa ni pambano linalotarajiwa kuwa kali na la kusisimua.
Mabingwa Watetezi Manchester City watavaana uso kwa uso na Swansea City.
Gillingham, ambao waliwatoa Watford Raundi ya Pili, watasafiri kwenda White Hart Lane kucheza na Tottenham.
Nao Nottingham Forest, wanaokipiga Championship, watakuwa wenyeji wa Washika Bunduki wa London Arsenal.
Droo nzima hii hapa
No comments:
Post a Comment