Rais
Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa
Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati
wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
“Vyombo
vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani
wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali
hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema
Rais Magufuli.
Aidha
amewataka wakurugenzi wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika
maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya
serikali katika halmshauri zao.
Pia
amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi
wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji
wa chini yao wasioendana na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka
yao kuwaweka sawa.
Rais
magufuli pia amewaagiza wakurugenzi hao kusimamia ilani ya uchaguzi ya
chama cha mapinduzi kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na
wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya
nchi yao na kuongezea kuwa viongozi wa juu wana imani kubwa sana nao
ndio maana hata wakachaguliwa kutoka katika watanzania hawa milioni 50.
Aidha
Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa
viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali
ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.
Mbali
na hayo pia amewataka wakurugenzi hao kubadilika kifikra na kuachana na
kuongoza kwa historia kwani wananchi wa sasa wamebadilika na hivyo
wafanye kazi kwa bidii ili kuwatimizia wananchi yale wanayotaka na hivyo
nchi itasonga mbele.
No comments:
Post a Comment