Maafisa wawili wa
timu ya Atlabara ya Sudan Kusini wameuawa katika machafuko yaliyotikisa
mji mkuu wa Juba kuanzia Alhamisi juma lililopita.
Shirikisho la
soka la Sudan Kusini limetangaza kuwa maafisa 2 wakuu wa mabingwa hao
watetezi wa ligi kuu ya Sudan Kusini walipigwa risasi na watu
wasiojulikana''Bwana William Batista na Leko Nelson walipigwa risasi usiku wa kuamkia jumamosi.'' alisema mkuu wa wa SFA bwana Chabur Goc.
Batista alikuwa katibu mkuu wa klabu hicho huku Nelson akihudumu kama meneja wa klabu hicho.
''Tunaomba mwenyezi mungu awaweke mahali pema peponi'' alisema bw Goc.
Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadha kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa makamu wa Rais Dkt Riek Machar.
Licha ya kutia sahihi makubaliano ya amani wafuasi wa viongozi hao wawili hawajaafikiana.
Vituo vya Umoja wa Mataifa pamoja na maeneo ya raia pia yameshambuliwa, jambo ambalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema huenda likawa uhalifu wa kivita.
Takriban watu 200 wengi wao wakiwa wanajeshi wameuawa katika machafuko hayo.
No comments:
Post a Comment