Friday, 8 July 2016

Kuna Mnigeria kauwawa Italia kisa ubaguzi wa rangi aliofanyiwa mke wake

BBC wameripoti kwamba Polisi wa Italia wamemshikilia Mwanaume mmoja anaetuhumiwa kumpiga hadi kumuua Muhamiaji mmoja raia wa Nigeria katika shambulizi la ubaguzi wa rangi. 
Emmanuel Chidi amekuwa akiishi Italia tangu mwaka 2015 ikiwa ni baada ya kutoroka vita nchini kwake Nigeria ambapo taarifa zinasema alivamiwa Jumanne alasiri kwenye mji wa Fermo alipokuwa akitembea na mke wake.
Imeripotiwa kwamba raia mmoja wa Italia alimtukana mke wa Chidi matusi ya kibaguzi, yakachochea mvutano ambapo raia huyo wa Italia Amedeo Mancini baadaye alimshambulia Chidi kwa kutumia chuma.
Chidi alifariki dunia siku moja baadaye na sasa Polisi wamemkamata mwanaume huyo na kumshtaki kwa makosa ya maauji yasiyo ya kukusudia ambayo yalichochewa na ubaguzi wa rangi.
Miongoni mwa waliohuzunishwa na tukio hilo ni Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi ambaye amesema Waitaliano wote wanapaswa kupinga ubaguzi wa rangi, sasa hivi wengi wanahofia huenda ikawa ishara ya taharuki inayotokana na wahamiaji wengi wanaopewa hifadhi kwneye nchi hiyo wakitokea Afrika

No comments:

Post a Comment