RIPOTI
zimeibuka kuwa Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia Mwaka Mmoja na
kumtwanga Faini ya Milioni 3 Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Yanga,
Jerry Muro.
Kikao
cha Kamati hiyo ya TFF kilifanyika Leo chini ya Wakili Wilson Ogunde
Jijini Dar es Salaam bila Muro kuhudhuria kwa vile alikuwa na udhuru
mwingine.
Muro
anadaiwa kudharau Maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF Mwaka 2015
alipoamriwa kulipa Faini ya Shilingi Milioni 5 alipokutwa na Hatia na
kutolipa Fedha hizo kitu ambacho Taarifa ya Mwenyekiti wa Yanga
alibainisha kuwa ilishalipwa.
Mengine
yaliyomsulubu Muro ni yale yaliyohusu kuelekea kwa Mechi ya Mashindano
ya CAF ya Kombe la Shirikisho ambayo Yanga waliamua Mechi hiyo iwe bure
kwa Mashabiki wote.
Hilo liliwakera TFF na Rais wao, Jamal Malinzi, kuitisha Mkutano spesho wa Waandishi wa Habari na kulizungumzia kitu ambacho kiliamsha hisi za Yanga kiasi ambacho Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, nae kutoa Taarifa ndefu na kali kuinanga TFF.
Kwenye Taarifa ya Manji, kuhusu Jerry Muro, ilisomeka:
2. KUITWA KWA JERRY MURRO KATIKA KAMATI YA MAADILI YA TFF AKIWA MKURUGENZI WA HABARI WA KLABU
2.1.
Hati za TFF za kuitwa kwa Jerry Murro hazionyesha wazi sababu ya
Mkurugenzi wa Habari huyo wa Yanga kutakiwa kufanya hivyo ambapo atakuwa
akihudhuria si kwa cheo chake katika klabu, lakini ifahamike wazi
kwamba Yanga haitakubali Mkurugenzi wake wa Habari afungiwe kushiriki
katika shughuli za soka. Tukiwa kama klabu tuko tayari hata kuunga mkono
hatua zozote za kisheria dhidi ya TFF na iwapo TFF itajaribu kuifungia
Yanga, tutalichukua suala hili hadi katika vyombo vya juu zaidi vya
michezo.
2.2. Hata hivyo, iwapo kuitwa huko kunahusu suala la faini ya Sh. 5 Milioni dhidi ya Jerry, fedha hiyo ilikwishatolewa kwa TFF.
2.3.
Wanaokula njama ndani ya TFF kuwanyamazisha au kuwafungia ambao
wanaeleza mawazo yao kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, lazima wafahamu
kwamba kuikosoa TFF hakupingani na sheria, na wafahamu pia kwamba Yanga
chini ya uenyekiti wangu haitakubali wanachama au wafanyakazi wa klabu
kudhalilishwa au kutishwa.
No comments:
Post a Comment