Thursday, 7 July 2016

Je, unajua kama kufunga ni moja kati ya zoezi linaloimarisha afya ya ubongo wako?

Wakati ndugu zetu waislamu duniani kote wakifunga mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, basi nimeona sio haba kama tutafahamishana mambo kadha wa kadha juu ya kufunga.duniani kote na dini zote zinahamasisha kufunga, hii sio kwa faida tu za kiimani bali ni pia kuna faida kedekede katika mwili wako.
Kufunga pia kunaweza kuwa ni desturi ya mtu binafsi vile utakavyo jiwekea, kama utafunga kwa kila mara mbili kwa wiki, kufunga kwa mara moja kwa mwezi au siku 30 kama katika mwezi mtukufu au unaweza chagua aina ya staili za ufungaji  kwa vile unavyoona ni raisi kwako.
Tukiachana na habari za kiimani kuna kufunga kwa kawaida au inaitwa “Intermittent fasting (IF)”, hii ni aina ya kufunga kula lakini pia unaweza kunywa vitu vya kimiminika kama maji,chai au kahawa.unaweza kufunga kwa masaa 8,12 hadi 24 yaani siku nzima. Na hapa tutaangalia faida za kufunga  katika mwili wa binadamu
1.Mabadiliko katika seli na homoni
Unapo acha kula kwa muda mwili wako unakuwa katika mabadiliko kadhaa, mwili wako husaidia kiwango cha Insulin kuwa sawa(balanced)  Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu.  Hii husaidia kutopata ugonjwa wa kisukari, mabadiliko kadhaa katika vina saba vyako, ambayo pia husaidia kuchochea kinga za mwili.
2.kupungua kwa uzito na kitambi
Kwa mtu anaefunga na kufwatilia vizuri masharti, funga humsaidia kupunguza mafuta mengi mwilini, na kupunguza kitambi, watu wengi wanaofunga hawawezi kula chakula kingi baada ya kufungua funga zao, kwahiyo kuna uwezekano wa kupungua kwa uzito kwa asilimia 3- 8 ndani ya wiki 3- 24 kama utafanya kufunga ni desturi na sio mpaka vipindi kama vya Ramadhani au Kwaresma basi kuna uwezekano wa kupungua uzito mwingi zaidi.
  1. Kujikinga na Kansa
Japokuwa bado wanasayansi wanafanyia uchunguzi swala hili baadhi ya utafiti uliofanyika kwa wanyama inaonyesha kufunga kwa takribani masaa 12 hadi 36 husaidia kuzuia hatari ya kupata ugonjwa wa kansa, kwani kufunga kuna faida kubwa katika metaboli ya mwili wako.
  1. Afya ya Ubongo wako
Unachokula  kinafika tumboni na pia kina umuhimu katika ubongo wako kufunga husaidia kuchochea ukuaji wa nuroni mpya katika ubongo wako na kusaidia kulinda ubongo na maradhi kama msongo wa mawazo,kupooza kwa mwili,ugonjwa wa Alzheimer pia kuimarisha ufanisi wa ubongo wako.
  1. kusaidia Kuongeza siku za Kuishi
Inaweza ikaonekana kama ni jambo la ajabu sana lakini kwa utafiti uliofanyika kwa baadhi ya wanyama, imeonekana wanaofunga mara kwa mara waliweza kuongeza siku zao za kuishi kwa asilimia 83%,  japokuwa uchunguzi bado unafanyika kutetea tafiti hizi. unaweza pia kusoma juu ya faida hizi kupitia tovuti  hii.

No comments:

Post a Comment