Viongozi wa chama mbadala AfD nchini Ujerumani Frauke Petry na Jörg Meuthen
Chama cha
mrengo mkali wa kulia cha AfD kimegawanyika baada ya mzozo
uliosababishwa na kauli iliyotolewa na mbunge wa chama hicho juu ya watu
wanaokana kutokea kwa maangamizi ya Wayahudi.
Kiongozi
mwenzi wa chama hicho, Jörg Meuthe, ameanzisha kundi lake.Mgogoro wa
chama hicho ulianza baada ya mbunge huyo Wolfang Gedeon kusema mwezi
uliopita kwamba ni halali kukana kutokea maangamizi wa Wayahudi kwa
sababu huo ni uhuru wa kutoa maoni.
Kiongozi
mwenza wa chama hicho cha mrengo mkali wa kulia anaewaongoza wabunge wa
chama hicho katika jimbo la Baden Württemberg kusini mwa Ujerumani,Jörg
Meuthen alitaka mbunge huyo, Gedeon afukuzwe chama , katika jimbo hilo
lakini bwana Meuthen hakufanikiwa kupata idadi ya kutosha ya wanachama
wa kumuunga mkono na ndio sababu aliamua kuunda kundi lake analoliiita
Chama Mbadala cha jimbo la Baden Württemberg.
Mgongano
ulitokea baina ya bwana Meuthen na Mwenyekiti mwenza wa chama cha AfD
Frauke Petry kutomlaani mbunge huyo alietoa kauli ya kuwaunga mkono watu
wanaokana kutokea kwa maangamizi ya Wayahudi. Kukana kutokea kwa
maangamizi ya Wayahudi Milioni sita ni kosa la jinai nchini Ujerumani
Hata
hivyo mbunge huyo ameamua kujiengua mwenyewe. Mwenyekiti mwenzi bibi
Frauke Petry amesema amefurahi kwamba bwana Gedeon amejiondoa mwenyewe
kutoka kwenye chama baada ya majadiliano ya saa kadhaa.
Bibi
Petry amesema anatumai kwamba mazungumzo zaidi yatafanyika na wanachama
wa jimbo la kusini mwa Ujerumani. Bibi Petry anatumai kwamba baada ya
mbunge huyo kuondoka mgogoro utatuliwa katika chama hicho cha mrengo wa
kulia.
Wanachama 12 wajitoa
Wanachama
12 katika jimbo la Baden Württemberg wamejitoa kwenye chama kikuu na
kujiunga na kundi jipya la jimbo hilo la kusini mwa Ujerumani.
Chama
Mbadala cha Ujerumani, AfD kimekuwa kinastawi katika umaarufu nchini
Ujerumani pia kutokana na mgogoro wa wakimbizi. Wakimbizi zaidi ya
Milioni moja wamewasili nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka mmoja
uliopita.
Chama cha
AfD kimefainikiwa kuingia katika mabunge ya majimbo sita kati ya 16 ya
nchini Ujerumani. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Ujerumani
wanasema mvutano wa kugombea mamlaka umezuka katika chama cha AfD baina
ya viongozi wenzi wa chama hicho kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini
Ujerumani.
Chama
hicho kilianzishwa mnamo mwaka wa 2013 kwa kampeni ya kuupinga Umoja wa
Ulaya lakini sasa kimegeuka kuwa hasa chama cha kuupinga Uislamu. Kwa
mujibu wa uchunguzi wa maoni, chama hicho kinaungwa mkono kwa asilimia
10 nchini Ujerumani.DW
No comments:
Post a Comment