Muonekano
Wapo wanaonekana na muonekano mzuri na wenye rangi nzuri za kuvutia na shukrani za dhati ziende kwa simu zote zilizo na kamera nzuri na Aina za application ambazo zinatumia kutengeneza rangi zetu kwenye simu. Wapo ambao ukikutana nao mitaani unaweza kimbia. Achilia mbali siku hizi kila dada mweupe, hakuna mtu anataka kuwa mweusi
Chakula
Wale wanaokula Pizza na vyakula vizuri vizuri tu kwenye migahawa ya bei za juu mjini,au mahoteli makubwa ya bei, wakionekana wanakula bata kila siku. hawa kila siku kwao sikukuu, kitu ambacho si kweli, na usipate sana tabu kuwaza lini utaweza kutembea kwenye mahoteli hayo kila siku kama wao.
Starehe Kila siku
Wapo wanaonekana wanatoka kila siku za juma Yaani jumatatu hadi jumatatu yeye anashereheka tu, sikataii wapo walio na pesa za kutumia na kustarehe kila siku ila pia sio kila anaepiga picha mbele ya jengo la samaki samaki basi alikuwepo wengine walipita tu kwa nje.
Mazoezi (Fitness)
Hapa tumeona watu wengi wamejikita kwenye swala la kufanya mazoezi ya mwili kama kupunguza matumbo na manyama uzembe, wanaume kutengeneza vifua wanaita six packs na mambo kama hayo wapo ambao utawaona wakijidai kufanya mazoezi hata na wataenda gym ila kutana nao mtaani ucheke hawabadiliki sababu wanafanya kwa kuonyesha tu kwenye mitandao
Kuwa kwenye Diet
Wengine utawaona wanajidai wakipost vyakula vinaonyesha wapo kwenye Diet, labda kwa kugeza wasanii kadhaa kadhaa wakifanya mambo hayo Wengine husema “Fake it till you make it”, sio kila kitu lazima tufanye waone, japokuwa uko huru kuweka chochote utakacho kugeza geza au kuigiza ndio maisha ya watu mjini.
Mahusiano
Ukiangalia picha za watu unaweza ukatamani aina ya maisha ya mahusiano wanayoishi ila sio wote wanaonekana wenye furaha kwenye hizo picha basi ni wana mapenzi yasiyo na matatizo utatamani hata uwe kama wao. kuna mapenzi ya mitandao ya kijamii mapenzi ya kujionyesha wakati mwingine sio kila unachokiona ni cha kweli.
Watoto na Wanyama
Wengine hujidai wanajali watoto katapiga picha na kuonyesha dunia nzima ila si kweli wanashinda na watoto nyumbani au hata wengine kutoa misaada kwa watoto yatima na picha kibao ili waonekane, au picha zao zinaonyesha kujidai wanapenda wanyama sana kama kuwajali mbwa au paka au aina yoyote ya wanyama wanaofugika nyumbani. ndo maana kuna wakati kila staa mbogo alionekana anafuga mbwa, lakini sahivi mbwa hawaonekani, kwanini sababu ilikuwa tu fasheni kwa mda. kwahiyo tujifunze kusoma alama za nyakati.
No comments:
Post a Comment