Ureno wamelazimishwa sare na Iceland wakati wa kampeni zao za kuwania taji la Mataifa ya Ulaya zikishindwa kufanikiwa kwa kupata ushindi dhidi ya timu ambayo haikupewa nafasi ya kuwazuia mastaa wa Ureno.
Gylfi Sigurdsson alipoteza nafasi ya kuipa Iceland bao la kuongoza baada ya shuti lake kuokolewa.
Nani akaifungia bao Ureno lakini Iceland wakapambana na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Birkir Bjarnason aliyepiga volley na kujaa moja kwa moja kambani.
Mpira wa kichwa uliopigwa na Cristiano Ronaldo uliokolewa dakika za lala salama huku Iceland wakikaribia nao kupata bao la ushindi lakini shuti la Alfred Finnbogason liliokolewa.
Iceland walikuwa wanacheza mchezo wao wa kwanza wa mashindano makubwa, licha ya Ureno kumiliki mpira kwa kwa asilimia nyingi lakini hawakufanikiwa kuchomoka na ushindi.
Ronaldo ameingia kwenye mashindano akiwa ametoka kufungia Real Madrid penai ya ushindi kwenye mchezo wao wa fainali ya Champions League dhidi ya Atletico Madrid na kuiongezea klabu yake idadi ya mataji ya UEFA Champions League.
Mataji akiwa na timu yake ya taifa yamemgomea, labda makali yake ya kutupia nyavuni akiwa Real Madrid ayahamishie kwenye kikosi cha taifa lake.
Ronaldo ambaye amefikisha mechi 127 na kufikia rekodi yam kali wa zamani wa Ureno Luis Figo, alikimbia kuiwahi krosi ya Nani lakini mpira aliopiga kwa kichwa akiwa ndani ya sita uliokolewa.
Dondoo muhimu
- Ureno wameshindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye mechi zao za ufunguzi za michuano mikubwa tangu mwaka 2008 (D2 L2).
- Renato Sanches amekuwa mchezaji mdogo zaidi kwenye timu ya Ureno kucheza kwenye mashindano makubwa (miaka 18 na siku 301) akivunja rekodi ya Cristiano Ronaldo (miaka 19 na siku 128)
No comments:
Post a Comment