Mitandao ya kijamii imeshinda televisheni kama chombo cha kusambaza habari kwa vijana ,kulingana na ripoti.
Vijana
wenye umri kati ya miaka 18-24 waliohojiwa , asilimia 28 walisema njia
yao ya kupata habari ni kupitia mitandao ya kijamii ikilinganishwa na
asilimia 24 kwa runinga.Chuo cha Taasisi ya Reuters cha Uandishi wa habari, pia kimependekeza kuwa asilimia 51 ya watu wenye uwezo wa kutembelea mitandao hutumia mitandao ya kijamii kupata habari
Ongezeko la utumizi wa simu za rununu ili kupata habari umekandamiza mfumo wa kibiashara wa hapo awali.
Katika ufunguzi wake , ripoti hiyo inasema ' pigo hili la pili ' imekuwa pigo kwa mashirika ya habari kote ulimwenguni na kuna uwezekano wa atahri kubwa kwa wachapishaji na wazalishaji habari katika siku zijazo.
No comments:
Post a Comment