Sunday, 19 June 2016

MESSI AMEIFIKIA REKODI YA MFUNGAJI WA MUDA WOTE ARGENTINA

Messi-Batistuta


Lionel Messi sasa ameifikia rekodi ya striker wa zamani wa Argentina Gabriel Batistuta aliyekuwa anakamatia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote.
Batistuta alitumia kambani bao 54 kwenye game 78 alizoichezea Argentina (lakini chama cha soka cha Argentina AFA hakihesabu magoli mawili ambayo alifunga dhidi ya Slovania wakati akiichezea timu ya vijana mwaka 1995) katika michuano ya kimataifa ambapo alianza kucheza tangu mwaka 1991 hadi 2002 na kufanikiwa kushinda mataji ya Copa Amerika mwaka 1991 na 1993 huku akifanikiwa kupiga hat-trick kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 1994 na 1998.
Lakini Messi, 28, sasa amefanikiwa kuifikia rekodi hiyo alipofunga goli dakika ya 60 wakati Argentina ikiichapa Venezuela kwa bao 4-1 kwenye uwanja wa Gillette huko Marekani na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya Copa America Centenario.
 “Nimeifikia, bado sijaivunja. Lakini ninafurahi kufikia rekodi ya Bati, inamaana sana,” alisema Messi baada kumalizika kwa mchezo.
Kocha wa timu ya taifa ya Argentina Gerardo Martino alisema: Nadhani anafasi ya kuweka rekodi yake. Nitafurahi kama itatokea kwenye michuano ya Copa America.”
Star huyo wa Barcelona aliyefikisha magoli 54, anafukuzwa kwa karibu na wachezaji wenzake Sergio Aguero (33) na Gonzalo Higuain (26).
Magoli 54 aliyoifungia Argentina, 27 yametokana na mechi za kirafiki, 15 yakiwa ni magoli aliyofunga kwenye mechi za kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia, mabao saba kwenye michuano ya Copa Amerika na magoli mengine matano amepachika kwenye fainali za kombe la dunia.
Messi alitokea benchi na kufunga hat-trick Argentina iliposhinda kwa goli 5-0 dhidi ya Panama kwenye michuano ya Copa America, kwa ujumla amefunga magoli tisa akiingia kutoka benchi wakati magoli 45 ameyafunga akiwa ameanza kwenye kikosi cha kwanza.
Katika bao hizo 54, amefuka hat-trick nne, magoli 6 (yakiwa ni magoli mawili (double) kwenye mechi moja, huku magoli 30 akiwa amefunga mojamoja (single). Magoli 42 amefunga kawaida (open play) wakati magoli 11 yametokana na mikwaju ya penati.
Brazil na Paraguay ndiyo timu pinzani zaidi dhidi ya Messi, amefunga mara nne dhidi ya timu zote mbili, huku akifunga mara tatu dhidi ya timu nyingine saba.
Alicheza mechi yake ya kwanza kwenye timu ya taifa ya Argentina akiwa na miaka 18, mchezo wa kirafikia dhidi ya Hungary mwaka 2005 lakini akalimwa kadi nyekundu dakika mbili baada ya kuingia akitokea benchi na ilichukua mechi sita kufunga goli lake la kwanza kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Croatia mchezo uliokuwa wa kirafiki.
Goli lake la kwanza kwenye mechi ya mashindano lilikuwa dhidi ya Serbia and Montenegro wakati Argentina inashinda kwa magoli 6-0 kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2006 lakini ilibidi asubiri hadi February 2012 kufunga hat-trick yake ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Switzerland alipoisaidia Argentina kupata ushindi wa magoli 3-1.
Mesi alikuwa mchezaji wa pili wa Argentina kufikisha magoli 50 mwezi March mwaka huu alipofunga kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Bolivia katika harakati za kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia.
Miaka miwili iliyopita, Messi ameisaidia Argentina kufika fainali ya michuano ya kombe la dunia na Copa America lakini bado hajashinda taji lolote kubwa akiwa amevaa uzi wa bendera ya Argentina.

No comments:

Post a Comment