Thursday, 9 June 2016

Hupendi kutumia Sukari? Zijue faida za asali kwenye mwili wako

Kwa miaka mingi asali imetumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali, ila najua wengi wetu tunajua tu kuipaka pale tunapo ungua na moto ila kuna faida zingine nyingi za asali wengi wetu hatuzijui au tu hatujaamua kujua faida zake.
Kama sukari ni tatizo kuipata unaweza ukafanya asali kama ndo sukari katika chai yako, achilia mbali utamu unaopatikana katika asali lakini pia asali ni dawa, unaweza itumia asali katika vitu tofauti tofauti, kwenye mkate, keki na vingine vingi.
asali
Faida za Asali Mwilini
Asali inasaidia kuchochea kumbukumbu kwa wale walio na matatizo ya kusahau sahau asali inasaidia sana kukufanya ukumbuke, Tunaweza kusema ina boost Kumbukumbu zako.
Matatizo ya kupata usingizi yanaweza kutibika kwa kutumia asali mara kwa mara, na inaweza kusaidia watu wanaopata matatizo ya usingizi na walale vizuri,asali pia ni dawa ya mba kichwani unaweza kuchanganya na maji ya moto na kupaka katika sehemu husika na kuiacha kwa muda kabla haujaiosha.
kwa wanawake wanaopenda urembo,Asali pia unaweza kuipaka usoni kwa muda na ukaitoa na kunawa na maji ya uvugu uvugu husaidia kun’garisha ngozi na kuifanya ngozi yako iwe na mvuto. kama unataka kutoka na unahisi uso wako haujakaa vizuri paka asali osha alafu paka vipodozi na utaonekana mrembo sana.
Nimeona watu wengi wakiangaika kupunguza matumbo na uzito kwa kutumia madawa, ambayo kiukweli hakuna anaejua Madhara yake baadae kwani madhara huwa hayaonekani kwa muda mfupi, wakati mwingine madhara huchukua miaka kuonekana,
Lakini  Asali, Ndimu na Maji ya Moto, inaweza saidia vitu vingi japokuwa baadhi ya watu wanadhani asali na ndimu ni sumu. Ila si kweli? Asali ukiiweka kwenye maji ya moto na kukamulia kipande cha ndimu ni dawa ya vitu vingi.
asa
kama Mmen’genyo wa chakula chako,Ukiwa unatumia Asali maji ya moto na ndimu, itasaidia (digestion ) mmen’genyo wako wa chakula utafanyika haraka zaidi na kukusaidia kutoka kuwa na kitambi,pia husaidia kupata choo kwa wale wanaopata tabu kupata choo.
Asali pia ni dawa ya mafua na Kikohozi,Kama una mafua na kifua cha kubana sana, tumia asali na maji ya moto kamulia ndimu, itakusaidia kufanya upumue vizuri.Tumia mara mbili au tatu kwa siku na utaona maajabu.
Asali pia husaidia Kutoa Sumu Mwilini na Mafuta,Wakati unaangaika kutafuta Dawa za kutoa sumu mwilini, tumia mchanganyiko huo, utashangaa unaenda sana chooni, kiukweli unaweza kuharisha sana kipindi cha mwanzo ukahisi unaumwa ila ndo jinsi uchafu au mafuta ya mwili wako yatakavyotoka mwilini, lazima uharishe, kwahiyo usishangae kupata safari nyingi za chooni.

No comments:

Post a Comment