Robo Fainali za Copa America Centenario zitaanza kuchezwa Usiku huu wa Leo huko Marekani.
Wenyeji USA ndio watafungua dimba kwa kucheza na Ecuador.
Jumamosi ni Peru na Colombia na Jumapili zipo Mechi mbili za mwisho
kati ya Argentina na Venezuela na kisha ni Mabingwa Watetezi Chile
kucheza na Mexico.
Ratiba
Robo Fainali
Ijumaa 17 Juni 2016
0430 USA v Ecuador [RF1]
Jumamosi 18 Juni 2016
0300 Peru v Colombia [RF2]
Jumapili 19 Juni 2016
0200 Argentina v Venezuela [RF3]
0500 Mexico v Chile [RF4]
NUSU FAINALI
Jumatano 22 Juni 2016
0400 Mshindi RF1 v Mshindi RF3
Alhamisi 23 Juni 2016
0300 Mshindi RF2 v Mshindi RF4
MSHINDI WA TATU
Jumapili 26 Juni 2016
0200
FAINALI
Jumatatu 27 Juni 2016
0300
SSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
DONDOO MUHIMU:
-Mashindano haya Copa América Centenario ni mahsusi kusheherekea
Miaka 100 ya Copa America, Mashindano ya Shirikisho la Soka la Nchi za
Marekani ya Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa Mwaka 1916.
-Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya Kusini.
-Haya yatakuwa ni Mashindano ya 45 kufanyika na kawaida yake
hufanyika kila baada ya Miaka Minne lakini safari hii CONMEBOL na
CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na
Nchi za Visiwa vya Caribbean, walikubaliana kuandaa Mashindano maalum.
-Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16, badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za CONCACAF.
-Kawaida Mshindi wa Copa America huiwakilisha Marekani ya Kusini
kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho lakini Mshindi wa Copa
América Centenario hatapewa hilo kwani Mwaka Jana Chile, wakiwa Nyumbani
kwao, ndio walitwaa Copa America ya kawaida na wao ndio watashiriki
Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho Mwakani, 2017, huko Russia.
SSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
**CONMEBOL:
-Argentina
-Bolivia
-Brazil
-Chile (Mabingwa Watetezi)
-Colombia
-Ecuador
-Paraguay
-Peru
-Uruguay
-Venezuela
CONCACAF
-Mexico
-USA
-Jamaica
-Costa Rica
-Haiti
-Panama
No comments:
Post a Comment