Ile hukumu iliyokuea inasubiriwa kwa hamu na wadau wa soka nchini, inayohusu upangaji wa matokeo wa ligi daraja la kwanza katika kundi C tayari imeshakamilika.
Mapema hii leo www.shaffihdauda.com iliibuka kwenye ofisi za TFF na kuweka kambi kutaka kujua ni kipi kitaamuliwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka ambayo ilikutana leo ikiahidi kutoa hukumu majira ya mchana.
Lakini ilipofika majira ya saa 7:00 mchana ilisogezwa mbele kwasababu hukumu ndiyo ilikuwa inaandikwa, lakini hata ilipofika majira ya saa 10:00 jioni bado hali ya kupata taarifa hizo ilikuwa ngumu na taarifa iliyotoka ilikuwa ni kwamba hukumu hiyo haiwezi kutoka leo hivyo watu wasubiri hadi kesho April 3 majira ya saa 4:00 asubuhi.
Uchu wa kutaka kujua nini kitatokea ukafanya shaffidauda.co.tz kuendelea kusubiri kupata huku hiyo, ilipotimu saa 10:20 Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu Jerome Joseph Msemwa akatoka na hapo nikataka kujua nini kimeamuliwa na kamati yake.
Lakinin hata hivyo, Mwenyekiti huyo akagoma kusema hukumu inasemaje huku akiahidi kwamba kesho ilakitu kitawekwa hadharani.
Na hii ndiyo ilikuwa kauli yake: “Hukumu iko tayari kabisa nin ndefu, ina kurasa zaidi ya 34. Hukumu itatolewa rasmi kesho tarehe 3 April 2016 saa 4:00 asubuhi kwenye ofisi za TFF.”
“Asilimia kubwa ya watuhumiwa walifika na kunawengine hawakufika waliandika barua na wachache ambao walikataa wito lakini hiyo haikuzuia kamati kuendelea na kesi”.
Kesi ambayo ilikuwa inasikilizwa leo ilikuwa inaihusu michezo miwili ya kundi C ya ligi daraja la kwanza. Mchezo wa kwanza ni kati ya Geita Sports dhidi ya JKT Kanembwa na mchezo mwingine ni kati ya Polisi Tabora dhidi ya JKT Orjoro.
Geita Sports na Polisi Tabora zote zilikuwa na nfasi ya kupanda ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao lakini michezo yao ya mwisho ikakumbwa na kashfa ya tuhuma za kupanga mazoteo kwasababu mchezo wa Geita Sports dhidi ya JKT Kanembwa ulimalizika kwa Geita kushinda kwa magoli 8-0 huku ule wa Poili Tabora dhidi ya JKT Orjoro ulimalizika kwa Polisi Kushinda kwa magoli 7-0.
Kama timu hizo zikikutwa na hatia huenda zikashushwa daraja na viongozi ambao watabainika na upangaji huo wa matokeo huenda wakafungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 10 pamoja na faini isiyopungua milioni 10 huku taratibu nyingine za kuwafikisha mahakamani zikichukua nafasi yake.
No comments:
Post a Comment