Profesa Omari Shaaban mtunzi wa 'Sina Makosa' |
Wimbo wa ‘Sina makosa’ ulitokana na kisa cha kweli. Kuna dada ambaye ni mzaliwa Kisumu aliyekulia Nairobi ndie chanzo cha hadithi ya wimbo huu, dada huyu aliyekuwa akifanya kazi Kenya Extelecoms kiwa na wadhifa mzuri hivyo maisha yake kuwa mazuri alikuwa mpenzi mkubwa wa Les Wanyika hapo ndipo akakutana na Profesa Omari na kuwa na urafiki wa siri kwani alikuwa pia na mapenzi na bwana mwingine aliyekuwa akifanya Special Branch ya usalama wa Kenya, huyu bwana alikua na familia yake pia. Siku moja Profesa na huyu dada wakiwa wamekaa katika Coffe Shop kwenye jengo la Kenya Cinema wakipata kinywaji ndipo huyu bwana wa Special Branch alipowakuta hapo na kuanzisha vurugu kubwa na kumpiga sana Profesa aliyeokolewa na wapenzi wa muziki waliomfahamu. Huyu mtu wa Special Branch nae alikuwa mpenzi mkubwa wa Les Wanyika, na baada ya kutoa adhabu hiyo alimwonya Profesa kuwa akiwakuta pamoja tena angemuuwa. Baada ya hapo jamaa alimuacha huyo bibi lakini binti aliendelea kuhudhuria maonyesho ya Les Wanyika hata wimbo huo ulipotungwa na kuwa maarufu..Hasira za nini bwanaa, wewe unawake nyumbani nami nina wangu nyumbani chuki ya nini kati yangu mimi na wewe, nasema Sina makosaa bwanaa……………….inaendelea
No comments:
Post a Comment