Hata
hivyo, akitangaza takwimu hizo jana, Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na
Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo
alisema; “hii inamaanisha kwamba kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na
ununuzi kwa mwaka ulioishia Februari ndiyo imepungua wala siyo kushuka
kwa bei. Naomba
lieleweke hapo. Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi
kwa Februari umepungua kutoka asilimia 10.7 ya Januari hadi 9.5
Februari,” alisema.
Kwesigabo
alisema kupungua kwa mfumuko huo kumechagizwa na kupungua zaidi kwa bei
za baadhi ya bidhaa ya vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi
kilichoishia Februari.
Alitaja
mwenendo wa baadhi ya bei za bidhaa zilizoonyesha kupungua kuwa ni gesi
asilimia 10.3, dizeli asilimia 4.5 na matunda asilimia 7.2.
No comments:
Post a Comment