Ikulu ya Marekani
imeiambia BBC kuwa Marekani inathamini sana uhusiano wake na Uingereza
,hayo yalisemwa saa chache baada ya Rais Obama kuikosoa vikali sera ya
mambo ya nje ya Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron.
Rais Obama
aliliambia jarida la "The Atlantic"kuwa Uingereza na Ufaransa
walisababisha Libya kufikia katika hali mbaya baada ya majeshi yao
kuingilia kati.Hata hivyo BBC imepokea maelezo mengine kutoka Marekani kupitia msemaji wa Ikulu Ned Price yanayomsifu Cameron kwa uongozi wake wa jumuiya ya kijeshi ya nchi za magharibi NATO.
Mhariri wa BBC America ya kaskazini amesema uongozi wa Obama unaonekana kuwa katika mkanganyiko mkubwa.
No comments:
Post a Comment