Wednesday, 9 March 2016

Al shaabab wazima makomando wa Marekani

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al shaabab walimezima shambulizi la kuvizia lililotekelezwa na makomando wa jeshi la Marekani usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa Afisa mmoja wa ngazi ya juu jeshini ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema kuwa shambulizi hilo lililotekelezwa na vikosi vya usalama la Marekani kwa ushirikiano na majeshi ya Somalia yalifanikishwa kwa kuruka kwa ndege za helikopta kwa kambi ya wapiganaji hao iliyoko Awdhegle, takriban kilomita 50 Kusini mwa Somalia.
Afisa huyo amethibitisha kuwa Makomando hao wa Marekani walihusika katika uvamizi huo.
Awali kundi la wanamgambo hao lilikuwa limesema kuwa lilizima shambulizi la kuvizia lililotekelezwa katika mojawepo ya kambi zao kwa njia ya helikopta.
 
 
Msemaji wa kundi hilo Sheikh Abdiasis Abu Musab aliiambia Reuters kuwa walimpoteza mpiganaji mmoja katika shambulizi hilo la usiku wa leo.
Wenyeji wa eneo hilo wanasema waliamshwa na milio ya risasi na ndege za kivita zikitua na kuondoka.
Shambulizi hili limetokea siku moja tu baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kushambulia kambi moja ya Al shaabab na kuuwa wapiganaji 150.
Alshabab ilipinga idadi hiyo ya wapiganaji ikisema kuwa nambari hizo zimeongezwa chumvi.
Sheikh Abdiasis Abu Musab amenukuliwa akisema kuwa hawakujua ni jeshi lipi lililotekeleza shambulizi hilo ila waliwazima.
 
 
''hatujui ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo''
''ndege hizo za helikopta zilitua kwenye mto Shabelle na makomando wakaanza kuvizia kambi yetu, hata hivyo tuliweza kuizima ila tulimpoteza mmoja wetu''
''Walikuwa wamebeba roketi na bunduki za M16 mojawepo ya bunduki maarufu sana na jeshi la Marekani.

No comments:

Post a Comment