Kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya wanawake wa AFGHANISTAN –
itakuwa timu ya kwanza ya soka ya wanawke kuvaa jezi ambazo
zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sheria za kidini
za nchi yao.
Jezi
hizo zitakuwa ni suruali za vitambaa laini na t-shirt ya juu ambayo
imeunganika na kiremba cha kichwani – hii nafanyika kutokana na sheria
za dini ya kiislamu ambazo zinamtaka mwanamke kujistiri kwa mavazi ya
namna hiyo.
Kucheza soka nchini Afghanistan kwa wanawake imekuwa sio jambo
jepesi, nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Khalida Popai alisema:
“Kucheza kunaweza kuwa hatari sana kwa wanawake hapa, nchi ambayo ina
mfumo dume kwenye maeneo yote. Haikuwa inaruhusiwa kucheza soka kwa
wanawake. Soka ni mchezo wa kiume.
“Hizi jezi ni zinaleta uhafadhali kwa wanawake wa taifa hili, na nina
furaha kuwa mfano bora kwa wasichana wadogo ambao wangependa kucheza
soka huko mbele.” I
No comments:
Post a Comment