Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza
|
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ameishukuru Benki ya MUKOBA[ PLC] kwa kuweza
kutoa msaada wa saruji yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane kwa wahanga wa mafuriko katika vijiji vya
tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini.
Bi
Masenza ameziomba taasisi mbalimbali kuweza kutoa msaada kwa wathilika wa
mafuriko kwani mahitaji bado ni mengi na wengi wao hawana makazi hadi sasa.
Kwa
upande wake Meneja wa Benki ya MUCOBA Bwana
Beni Mahenge amesema kuwa wao kama benki ambao wamekuwa wakiwahudumia
wananchi wameguswa na jambo hilo lililowakuta wananchi wa Tarafa ya Pawaga
nakufikia hatua ya kutoa msaada huo wa saruji yenye thamani ya shilingi milioni
moja na laki nane.
No comments:
Post a Comment