Polisi
jijini Mwanza wamewatawanya wananchi kwa mabomu katika eneo la Sinai,
Mtaa wa Nyerere ‘A’ Kata ya Mabatini baada ya kutokea vurugu kutokana na
mtu mmoja kugongwa na gari.
Polisi
walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu hao wakati
wakimuokoa dereva wa gari namba T. 520 CBM Mark X, Lifaty Dickson ambaye
alimgonga mtoto wa miaka sita, Festo William.
Hatua
hiyo ilifikiwa baada ya wananchi kuhisi kwamba polisi walitaka
kumtorosha dereva huyo kwa madai ya kufanya ajali bila kukusudia.
Wananchi
wanadai dereva huyo alifanya ajali baada ya kuendesha kwa mwendo kasi
na hatimaye kumgonga na kumsababishia mauti motto huyo aliyekuwa Mkazi
wa Kata ya Mahina.
“Mimi
nilikuwa katika eneo hili la ajali ilipotokea, sasa huyu mtoto
aliyefariki (Festo William) alikuwa anavuka katika eneo la watembea kwa
miguu, zebra lakini huyu mwenye gari alishindwa kupunguza mwendo.
“Baada
ya kuona hivyo sisi kama wananchi wapenda haki tulianza kumuadabisha
huyu mtu lakini polisi wakaingilia kati na sisi hatukukubali,“ amesema shuhuda mmoja aliyetambulika kwa jina la Simon.
Justus
Kamugisha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kudai kuwa, polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi
kumuokoa dereva wa gari hilo ambaye alikuwa akishambuliwa na wananchi.
Kamugisha
amesema kuwa, polisi wake walishambuliwa kwa kupigwa mawe na wananchi
hao, hivyo hawakuwa na njia yeyote ya kujiokoa tofauti na kutumia mabomu
ya machozi.
“Polisi
hawakuwa na njia yoyote tofauti na hiyo, waliamua kufanya hivyo ili
kumuokoa dereva wa gari hilo na kuokoa raia wema wengine,” amesema Kamugisha na kuongeza kuwa watu watatu wanashikiliwa na polisi kutokana na mkasa huo.
No comments:
Post a Comment