BILA kutegemewa Kijana wa Miaka 18, Marcus Rashford, aliekuwa kapangwa Benchi alilazimika kuanza Mechi hii na hakutetereka kwa kuifungia Manchester United Bao 2 walipoishindilia FC Midtjylland Bao 5-1 na kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI kwa Jumla ya Bao 6-3 baada ya kupoteza Mechi ya kwanza 2-1.
Kabla ya Mechi kuanza Man United walipata pigo kubwa baada ya Anthony Martial, ambae alipangwa kuanza Mechi hii, kuumia wakati akipasha moto na nafasi yake kuchukuliwa na Chipukizi Marcus Rashford ikiwa Mechi yake ya kwanza kabisa kuchezea Timu ya Kwanza.
Pigo hilo lilifanya Benchi la Akiba la Man United kubakia na Wachezaji wa Akiba 6 tu kwenye Benchi badala ya wale 7 wanaotakiwa kuwepo.
FC Midtjylland walitangulia kufunga Dakika ya 28 kwa Bao la Pione Sisto lakini Dakika 4 baadae Bodurov alijifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa Krosi ya Memphis.
Dakika ya 42 Man United walipewa Penati kutokana na Andre Romer kumuangusha Herrera lakini Juan Mata alipiga mkwaju wa Penati hiyo kidhaifu na Kipa Andersen kuokoa.
Hadi Mapumziko Man United 1 FC Midtjylland 1.
Dakika ya 64 pasi ya Juan Mata ilimkuta Marcus Rashford aliefunga na kuwapa Man United uongozi wa Bao 2-1.
Dakika ya 75, si mwingine tena bali Kijana mpya wa Kitaa, Marcus Rashford, aliepiga Bao la 3 kwa kuunganisha Krosi ya Varela.
Herrera aliipa Man United Bao la 4 kwa Penati katika Dakika ya 88 na Memphis kushindilia Bao la 5 Dakika ya 90.
Man United sasa wamesonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na watamjua mpinzani wao Kesho Ijumaa Februari 26 baada ya Droo itakayofanyika huko Nyon, Uswisi.
VIKOSI:
Manchester United: Romero; Varela, Carrick, Blind, Riley; Schneiderlin, Herrera; Lingard, Mata, Memphis; Marcus Rashford
Akiba: J. Pereira, Rojo, Poole, McNair, Love, A. Pereira
FC Midtjylland: Andersen, Romer, Hansen, Bodurov, Novak, Sparv, Poulsen, Olsson, Hassan, Sisto, Urena
Akiba: Pusic, Kadlec, Dahlin, Banggaard Jensen, Bak Nielsen, Onuachu, Royer
REFA: Istvan Vad (Hungary)
Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumatano Februari 24
Sporting Braga 2 Sion 2 [Bao 4-3 kwa Mechi mbili]
Alhamisi Februari 25
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2
Lokomotiv Moscow 1 Fenerbahce 1 [1-3]
Athletic Bilbao 1 Marseille 1 [2-1]
Rapid Vienna 0 Valencia 4 [0-10]
Liverpool 1 Augsburg 1 [0-0]
Krasnodar 0 Sparta Prague 3 [0-4]
Lazio 3 Galatasaray 1 [4-2]
Schalke 0 Shakhtar Donetsk 3 [0-3]
Bayer Leverkusen 3 Sporting Lisbon 1 [4-1]
Molde 1 Sevilla 0 [1-3]
Napoli 1 Villarreal 1 [1-2]
Porto 0 Borussia Dortmund 1 [0-3]
Olympiacos v Anderlecht [0-1]==Mechi inakwenda Dakika za Nyongeza 30 Olympiacos wakiwa na Bao 1-0
Tottenham 3 Fiorentina 0 [4-1]
Basle v St Etienne [2-3]
Manchester United 5 FC Midtjylland 1 [6-3]
KALENDA
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi
No comments:
Post a Comment