Thursday, 25 February 2016

CAF yakutana na viongozi wa soka Afrika

Kamati kuu ya Shirikisho la kandanda la Afrika (CAF) linafanya mkutano wa dharura na wenyeviti 54 wa mashirikisho ya kandanda wa mataifa ya Afrika mjini Zurich Uswisi siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu wa urais wa shirikisho la soka duniani FIFA.Moja kati ya mada kuu itakayojadiliwa katika mkutano huu ni mapendezo ya mabadiliko katika Fifa baada ya ufichuzi wa sakati ya hongo ilimnasa rais Sepp Blatter na viongozi wengine wakuu wa FIFA.
Vile vile kuna hoja kubwa ya uwazi uadilifu wa viongozi na mbinu za kusimamisha ubadhirifu wa fedha zilizotengewa ustawi wa mchezo huo barani Afrika.
Aidha maswala ya kuwepo kwa sauti ya wanawake na uwakilishi wao katika kamati kuu zinazoendesha soka barani Afrika.
Shirikisho la soka la Afrika CAF hata hivyo linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa afisi kadhaa za mataifa ya Afrika.
CAF vilevile inatarajiwa kumnadi mgombea wa urais wa FIFA wanaomuunga mkono ambaye ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa kutoka Bahrain.

No comments:

Post a Comment