Buyern Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen Robben akaandika bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha pili.
Kwa upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.
Michuano hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man City huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi dhidi ya Atletico Madrid.
No comments:
Post a Comment