Saturday, 9 January 2016

Sheria kali za uhamiaji Ujerumani

Kansela Angela Merkel akizungumzia mkutano wa chama chake cha CDU alipokutana na waandishi wa habari. (09.01,2016)
Kansela Angela Merkel akizungumzia mkutano wa chama chake cha CDU alipokutana na waandishi wa habari. (09.01,2016)
Kansela Angela Merkel amesema Jumamosi (09.01.2016) kwamba anataka kuwepo kwa sheria kali za uhamiaji nchini Ujerumani baada ya mashambulizi kadhaa ya ngono mjini Cologne na katika miji mengine kulifadhaisha taifa
Akizungumza baada ya mkutano miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama chake cha Christian Demokrat (CDU) mjini Mainz Merkel amesema " Kile kilichotokea katika mkesha wa mwaka mpya ni vitendo vya uhalifu vya kukirihisha ambavyo vinahitaji kuchukuliwa hatua kali."
CDU mojawapo ya chama tawala nchini Ujerumani imechukuwa hatua hiyo ya kuimarisha sheria ya waomba hifadhi kufuatia mashambulizi makubwa ya ngono dhidi ya wanawake katika mkesha wa mwaka mpya mjini Cologne.
Chama hicho kimelipa kipaĆ¼ mbele suala la kuharakisha kurudishwa makwao watafuta hifadhi wanaotenda uhalifu nchini katika mpango wao vipengele kumi juu ya mustakbali wa Ujerumani.
Rasimu ya mpango huo wa CDU inajumuisha sheria mpya ambayo itamvuwa mhamiaji hadhi ya kupatiwa hifadhi baada ya kufanya kosa moja la uhalifu.
Hatua hiyo yumkini ikazusha majibu ya moja kwa moja kutokana na taarifa kwamba baadhi ya wanaume waliokamatwa kuhusiana na udhalilishaji wa kingono mjini Cologne kwa kweli walikuwa ni wahamiaji wanaomba hifadhi ukweli ambao ulifichwa kwa sababu za kisiasa.
Wakimbizi kupoteza haki ya ukaazi
Merkel amesema "iwapo mkimbizi anavunja sheria lazima kuwepo na taathira yake, hiyo ina maana wanaweza kupoteza haki yao ya ukaazi hapa nchini bila ya kujali anakabiliwa na kifungo cha nje au cha gerezani

No comments:

Post a Comment