Monday, 11 January 2016

Kamati za Bunge kukutana Dodoma

Image result for ndugai bungeni
KAMATI za Bunge zitatangazwa Januari 20 mwaka huu na zitafanya vikao vyake mjini Dodoma, kabla ya kikao cha Bunge kitakachoanza Januari 26. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, jijini Dar es Salaam jana, ilisema tayari Spika wa Bunge, Job Ndugai amewateua Wabunge 15 kuunda Kamati ya Kanuni ya Bunge. Hiyo ni kamati ya kwanza kuundwa na kiongozi huyo mpya wa Bunge.
Taarifa hiyo ilisema kamati hiyo imeundwa na kutangazwa kabla ya Kamati nyingine, ili ifanye marekebisho ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge kuhusu majukumu ya kamati nyingine za Bunge kwa kuyashabihisha na majukumu ya Serikali kwa kuzingatia Muundo wa Baraza la Mawaziri lililopo sasa.
“Lengo kuu ni kuleta urahisi, ufanisi na tija kwa Bunge katika kuisimamia na kuishauri Serikali. Kamati zingine kwa mujibu wa taarifa hiyo zitatangazwa Januari 20 mwaka huu na zitafanya vikao vyake mjini Dodoma kabla ya kikao cha Bunge kuanza Januari 26” ilisema taarifa hiyo ya Bunge.
Kwa msingi huo, taarifa hiyo ilisema Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ambayo Spika ndiye Mwenyekiti wake na Naibu Spika ni Makamu Mwenyekiti, Kiongozi wa Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni Wajumbe kwa nyadhifa zao, itakutana katika Ofisi ya Bunge Ijumaa, Dar es Salaam.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Mwera, Makame Kassim Makame (CCM), Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ( Chadema), Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza (CCM), Mbunge wa Malindi Ally Saleh Ally (CUF), Mbunge wa Kaliua Magdalena Sakaya (CUF) na Mbunge wa Viti Maalumu, Salome Makamba (Chadema).
Wengine ni Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Jasmine Bunga (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu Zainab Athuman Katimba (CCM), Mbunge wa Muheza Balozi Adadi Rajab (CCM), Mbunge wa Buchosa Dk Charles Tizeba (CCM) na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM).
Taarifa hiyo iliwataka wabunge wote wawe wamefika Dodoma Januari 20, mwaka huu tayari kwa kuanza kwa Kamati za Bunge na Mkutano wa Bunge

No comments:

Post a Comment