Maranyingi tumekua tukisumbuliwa na matatizo kadha wa kadha katika mahusiano yetu na miongoni mwa changa moto zinazo sumbua watu wenh=gi nai pamoja na tatizo la marafiki na hata ndugu kuingilia mahusiano na kusababbisha ukakasi katika sukari
zifuatazo ni njia chache za nanmna ya kuzuia watu wasi ingilie penzi lako
1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:
Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa
nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza
unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha
kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza
kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala
mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili
kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
2. Upekee wa mambo: Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza
kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni
kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea
yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili,
utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo
katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.
3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa
kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana
watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe
mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua.
4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya
haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine
habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha
wengine kwa haraka unajinyima nafasi ya
kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa
kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo
ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya
tatizo.
5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu:
Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano
yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa
nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za
kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka
kuwashirikisha watu wengine.
No comments:
Post a Comment