KATIKA MKUU WA FIFA ALIYESIMAMISHWA, JEROME VALCKE |
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) iliyokutana
Disemba 15 mwaka jana, imeiagiza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia
kuilipa Simba SC ya Tanzania fedha za uhamisho wa mchezaji Emmanuel
Okwi ndani ya siku sitini (60) kuanzia Januari 7, 2016.
Katika
taarifa hiyo ya Fifa na nakala yake kutumwa kwa TFF, Etoile du Sahel na
Simba SC, Kamati ya Nidhamu imefikia uamuzi huo baada ya klabu ya
Etoile du Sahel kupuuza kuilipa klabu ya Simba SC kiasi cha dola za
kimarekani 300,000 za uhamisho wa mchezaji wa Emmanuel Okwi uliofayika
Januari 2014.
Katika
barua hiyo ya maamuzi ya kikao hicho, Kamati ya Nidhamu imesema baada
ya siku sitini (60) zilizotolewa kwa klabu ya Etoile kuwa imeilipa Simba
SC kumalizika bila malipo hayo kuwa yamaefanyika, wataagiza Etoile du
Sahel kukatwa pointi sita katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Tunisia.
Na
kama klabu ya Etoile itashindwa kulipa deni hilo hata baada ya kukatwa
pointi sita, Kamati ya Nidhamu ya Fifa itaamua kuishusha daraja klabu
hiyo kutoka Ligi Kuu mpaka ligi daraja la kwanza.
Chama
cha Soka nchini Tunisia (FTF) kimekumbushwa kutekeleza maelekezo hayo ya
Kamati ya Nidhamu ya Fifa ya kuipokonya pointi sita Etoile du Sahel, na
endapo FTF itashindwa kufanya hivyo basi itafungiwa kujishugulisha na
shughuli zote za mpira zinazosimamiwa na Fifa.
Aidha
Kamati ya Nidhamu ya Fifapia imeigiza klabu ya Etoile du Sahel kulipa
faini ya dola za kimarekani 20,000 ndani ya siku sitini (60) baada ya
kupokea uamuzi huo wa kamati.
TFF
imepewa jukumu la kuhakikisha Simba inalipwa deni hilo ndani ya muda
uliopangwa wa siku sitini (60) na endapo klabu ya Etoile du Sahel
itashindawa kufanya hivyo basi TFF iitarifu kamati ya nidhamu ya Fifa
juu ya suala hilo.
Kikao
hicho cha Kamati ya Nidhamu kiliiongozwa na Mwenyekiti Claudio Sulser
(Uswisi), Makamu Mwenyekiti Kia Tong Lim (Singapore), na mjumbe Fiti
Sunia (Visiwa vya Samoa)
No comments:
Post a Comment