Thursday, 7 January 2016

Diamond kuachia Collabo yake na Aka mwezi huu


Baada ya Utanipenda kazi inayofata ni collabo ya Diamond na rapper wa Afrika kusini, Aka.
JOHANNESBURG, SOUTH AFRICA – DECEMBER 11(SOUTH AFRICA OUT): AKA and Diamond Platnumz at the BET Experience Africa press conference on December 11, 2015 at the Radisson Blue Hotel in Johannesburg, South Africa. The inaugural BET Experience Africa is set to take place at the Ticketpro Dome this Saturday, December 12, 2015. (Photo by Lefty Shivambu/Gallo Images/Getty Images)
“Nadhani mwezi huu [January] tuna collaboration na AKA ambayo video yake ipo tayari,” meneja wa Diamond, Sallam ameiambia Bongo5.
Amesema sababu ya kuchelewa kuiachia japo waliahidi kuachia video mbili mwezi uliopita ni kwasababu wimbo ‘Utanipenda’ unafanya vizuri , Pia amesema wanauachiawimbo huo  kwasababu ni wakuparty ukizingatia ‘Utanipenda’ ni wa huzuni
“Tuna stock nyingi na hii ni collaboration, yaani ni nyimbo ya AKA na Diamond kwahiyo tunapotoa nyimbo ya collabo mara nyingi huwa tunasupport kuhakikisha kuwa inapita, sio unafanya halafu unaiacha tu.” Ameelezea Sallam.
Mwezi uliopita Diamond alishoot video ya collabo yake na Mafikizoro japo bado hawajatangaza itatoka lini.

No comments:

Post a Comment