Wananchi
wa kijiji cha Lukani katika Kata ya Ngu’ruhe wilaya ya kilolo mkoa wa Iringa wamemkataa
mtendaji wa kijiji hicho katika mkutano wa kijiji uliofanyika kijijini hapo
kutokana na utendaji mbovu wa kiongozi huyo.
Tukio
hilo limetokea katika mkutano wa hadhara
ulioudhuriwa pia na mbunge wa jimbo la Kilolo VENANCE MWAMOTO,diwani wa kata
hiyo, mwenyekiti na viongozi mbalimbali pamoja na wanakijiji.
Wananchi
wa kijiji cha Lukani wamesema mtendaji huyo ameshindwa kusimamia wananchi kupata
pembejeo za kilimo pamoja masuala mbalimbali ya maendeleo ya kijiji hicho.
Kwa
upande wake Mtendaji anayelalamikiwa NIKODEMASI KADINDE amesema yeye anafanya
kazi kwa ufanisi lakini kuna baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji wanapandikiza
chuki dhidi yake kwa wananchi wa kijiji hicho
Naye
diwani wa kata ya Ngu;ruhe PANCRASI KIHANGA amewataka wananchi kumvumilia
mtendaji wa kijiji hicho ili aweze kukabidhi nyaraka za serikali na baada ya
hapo watamuhamisha kikazi.
No comments:
Post a Comment