Askofu Telesphor Mkudewa Kanisa Katoliki, Jimbo la Morogoro, |
Akihubiri kwenye ibada ya misa takatifu ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice ,mjini Morogoro, Askofu Mkude alisema utaratibu huo utasaidia watoto wengi ,wakiwemo wa familia masikini kupata elimu bila kikwazo.
“Mimi binafsi nakubaliana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk Magufuli kwa hatua yake ya kutoa elimu bure jambo linalopaswa kuungwa mkono na wengi,” alisema Askofu Mkude.
Aidha aliipongeza serikali kwa hatua mbalimbali inazochukua zinazolenga kujali watu wanyonge. “ Watanzania wenzangu tumwombee Rais ili aweze kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa uaminifu zaidi,” alisema Askofu Mkude.
Alisema Magufuli amekuwa akifanya mambo mengi ya manufaa kwa taifa tangu alipoapishwa kuwa Rais, hivyo anapaswa kuungwa mkono zaidi. Askofu Mkude alisema, licha ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu kutokana na vyama vya siasa kuweka mbele utaifa, alishauri hali hiyo iendelee kufanyika kwa amani na maelewano upande wa Zanzibar. Alivitaka vyama vyote vya siasa visiwani Zanzibar viendelee kutanguliza maslahi ya taifa kuwepo uelewano.
No comments:
Post a Comment