Tuesday, 29 December 2015

USHIRIKIANO MBAYA CHANZO CHA KUSHUKA KWA SOKA IRINGA

  Image result for abu majeki

Ni takribani miaka kumi na moja sasa clabu ya lipuli haijashiriki ligi kuu Tanzania bara kitu ambacho kinawashangaza sana wadau wa soka mkoani Iringa.
Na msimu uliopita hiyo ilishindwa kupanda kutokana na migogoro ambayo ilikuwepo kati ya viongozi, kikundi kilichofahamika kama amusha popo. pamoja na wanachama, pia kunawengine ambao hata walidiliki kutupia lawama zao kwa viongozi kutokana na utendaji wa mbovu.
miongoni mwa kiongozi ambaye walimtupia lawama ni pamoja na mwenyekiti wa timu ya lipuli Abu Changawa Majeki ambaye alilaumiwa kwa utendaji wake hafifu katika masuala ya soka.
Wapenzi wa soka mkoani Iringa wanashauku kubwa sana kuona timu yao inakuwa na maendeleo ya kusonga mbele na kufikia hatua ya kushiriki ligi ya Tanzania bara.
Kujua zaidi sababu za kudorola kwa soka la mkoa wa iringa mwandishi wa mtandao huu wa HABARIKATZ alilazimika kumtafuta mwenyekiti wa clabu ya lipuli Abu Changawa Majeki na mahojiano yalikuwa hivi...
 Absalumu calosi : Mwenyekiti clabu ya lipuli kwa sasa inaonekana kutofanya vizuri na chanzo kikubwa ni migogoro hili unalizungumziaje.
Abu Majeki : Clabu ya lipuli kwa sasa haina migogoro na ni watu tu wachache ambao hawaitakii mema clabu yetu ndiyo maana siku zote wanaisemea vibaya.
Absalumu calosi : Kwa sasa uongozi wako umekuwa ukituhumiwa sana kuchangia kudorola kwa soka hili likoje mwenyekiti.
Abu Majeki : kiukweli uongozi upo imara ukiongozwa na mimi mwenyewe na mimi siku zote huwa nasema mkoani iringa mimi ni mtu wa kuigwa kwani nimeanza kujihusisha na soka kwa mda mrefu sana kwa hiyo ni mtu mzoefu na soka la mkoa wa Iringa.
Absalumu calosi : ushirikiano na wanachama ukoje mwenyekiti.
Abu Majeki : wanachama hawana mchango wowote ule tunawanachana wa maneno na si kutoa mchango katika soka na ndiyo maana nimefikia uamuzi kama mwenyekiti wa kuwafuta wanachama wote na kubaki na wanachama watano tu.
Absalumu calosi : mwenyekiti na ushirikiano kutoka serikalini ukoje hadi sasa
Abu Majeki : ushirikiano kutoka serikalini ni sawa na hakuna kwani watu wanahusika na michezo serikalini hawaoneshi jitihada zozote za kuendeleza soka mkoani Iringa
Absalumu calosi : kwa sasa mikakati yenu nini mwenyekiti
Abu Majeki mikakati yetu kwa sasa ni kuifanya clabu ya lipuli kuwa kama kampuni ili iweze kujitegemea na kufanya kazi kama kampuni
  

No comments:

Post a Comment