Rais wa Nigeria,
Mohammadu Buhari, ameiambia BBC kuwa majeshi yake yanakaribia kulishinda
kundi la kiislam , Boko Haram. Rais Buhari ameeleza kuwa kundi hilo
halina uwezo tena wa kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali
ama maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kwamba visa vya kujitoa
muhanga vimepungua .
Buhari ameeleza kuwa kundi hilo awali
lilikuwa na umoja ingawa kwa sasa limesambaratishwa vibaya katika
majimbo ya Adamawa na Yobe na kusalia katika jimbo la Borno ambayo ndiyo
ngome yao kuu .
Boko Haram wanaripotiwa kuendesha mashambulizi
zaidi ya mia moja na kuua watu zaidi ya elfu moja katika kipindi cha
miezi miwili iliyopita .
Ikumbukwe kwamba ,wakati wa kampeni zake
kuelekea uchaguzi nchini Nigeria,Rais Buhari alitoa ahadi ya kupambana
na kundi la Boko Haram mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment