Wakulima,wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda mkoani Iringa
wameshauriwa kutoa ushilikiano pale wanapohitajika kwaajiri ya kujadili kero
zinazowakabiri.
Hayo
yamesemwa na afisa mtendaji wa TCCIA mkoa wa Iringa BW. Jemes Sizia wakati
akizungumza na radio country fm ofisini kwake na kuongeza kuwa malengo
waliyonayo kwa sasa ni kuanzisha mabaraza ya biashara katika mkoa na wilaya ili
kuweza kusaidia kutatua kero mbalimbali kwa wafanyabiashara, wakulima na
wamiliki wa viwanda.
Aidha Jemes
amesema mabaraza yatakayo anzishwa yatasaidia kuwa na mazingira rafiki kwa
wafanyabiashara ambapo itasaidia kuboresha biashara zao na kuboresha ulipaji wa
kodi kwa serikali.
Pia Jemes
amesema serikali nayo inanafasi kubwa ya kushilikiana na tahasisi mbalimbali
nchini kwa kuondoa vikwazo na kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara
ili waweze kunufaika na kazi zao na kuondoa suala la kuyonywa kwa
wafanyabiashara.
Hata hizo
TCCIA wanampango wa kuendeleza kampeni
ya matumizi sahihi ya mizani na vipimo kwa wakulima na wafanya biashara hasa kwa nchi nzima
No comments:
Post a Comment