Moto wa Rais John Magufuli, umeendelea kuwababua vigogo serikalini ambapo safari hii Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Diwani Msemo, amesimamishwa kazi.
Taarifa iliyotumwa iliyosainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kusambazwa kwa vyombo
vya habari jijini Dar es Salaam jana ilisema Dk. Msemo amesimashwa kazi
kutokana na mgongano wa kimaslahi kufuatia manung’uniko kutoka kwa
wapokea huduma katika taasisi hiyo.
Taarifa ilisema Dk. Msemo amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi
pamoja na mambo mengine, kubaini iwapo mgongano wa kimaslahi umeathiri
utendaji kazi wake.
Aidha, Bodi ya taasisi hiyo imeagizwa kuteua mtu wa kukaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Msemo.
Hali kadhalika, taarifa hiyo ya Waziri imetoa siku 21 kwa
watendaji wote wa serikali katika sekta ya afya hususan wakuu wa vituo
vya kutolea huduma za afya, kukiri kwa maandishi kwa ngazi zao za
uwajibikaji endapo wanamiliki hospitali, zahanati, kliniki na maduka ya
dawa.
Ilisema Wizara ina jukumu la kusimamia utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuzingatia sera ya Afya ya mwaka 2007.
Aidha, taarifa ilisema katika ziara Waziri kukagua utoaji wa huduma
za afya katika maeneo mbalimbali, suala la upungufu wa dawa
limeendelea kujitokeza.
Nipashe ilimtafuta Dk. Msemo kumuuliza taarifa za kusimamishwa kazi
alijibu: “Sijapata taarifa hizo ndiyo nazisikia kutoka kwako...kwa sasa
niko Arusha kuhudhuria mkutano tangu juzi,”
chanzo;nipashe
No comments:
Post a Comment