Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 19 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania. Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Dar Es Salaam Young African waliwakaribisha Stand United chama la wana kucheza mchezo wao wa 12 wa Ligi.
Mchezo ulianza kwa Yanga kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa ila ndani ya kipindi cha kwanza Stand United walionesha uhai kwa kujitahidi kutaka kumiliki mpira ila Yanga walizidi kuwa makini na dakika 19 Thabani Kamusoko akatoa pasi nzuri kwa Amissi Tambwe na kupata goli la kwanza. Yanga walizidi kuwa mahiri na kuendelea kucheza kwa nidhamu.
Amissi Tambwe kwa mara nyingine tena alipachika goli la pili kwa Yanga dakika ya 37, kabla ya dakika 8 mbele kufunga goli la tatu baada ya kutumia vizuri pasi ya Donald Ngoma na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3-0, huku Tambwe akiwa kafunga hat-trick. Kipindi cha pili Yanga walipata goli lingine kupitia kwa kiungo wao wa kimataifa wa Zimbabwe Thabani Kamusoko dakika ya 63, baada ya kupiga kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Deus Kaseke dakika ya . Hadi dakika 90 zinamalizika Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo December 19
- Toto Africans 1 – 1 Simba
- Mwadui FC 2-1 Ndanda FC
- Kagera Sugar 1-0 Africans Sports
- Prisons 0-0 Mtibwa Sugar
No comments:
Post a Comment