Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya lori hilo lenye namba za usajili T 616 BEF aina ya Scania lilokuwa na tela namba T 320 BEF kupasuka tairi la mbele na hatimaye kulivaa basi hilo lenye namba T483 CTF.
Alisema majina ya watu waliofariki ambao kati yao, wanaume wako nane na wanawake wanne hayakuweza kupatikana mara moja na kwamba utambuzi unaendelea.
Aliwataja majeruhi waliokimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Michael Mahenge (40), Hawadi Msigwa (27) na Eliud Kalinga (20) wote wakazi wa Tunduma, Nicholaus Charles (45) mkazi wa DSM, Lulu Norbeth (15) na Anton Mwashiuya (43) wakazi wa Mbozi, Mbeya.
Wengine ni Juma Wiliam, Lucas Wilian, Willson Ndumba, Anitha Obadia Sanga, Arapha Hamdan, Razak Ngai na James Duma (49) raia wa Afrika Kusini. Majeruhi wengi ni Jonas, Kasungu Kabanga raia wa Congo, Frank Kalinga, Silverster Ndenye, Aizack Ndula, Lulu Ndula na Suma Japhet.
Naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk Museleta Nyakiroto alithibitisha kupokea kwa miili ya marehemu na majeruhi. “Kweli nimepokea miili ya marehemu 12 na tunaendelea kufanya utambuzi na majeruhi 28 ambao pia tunaendelea na utambuzi wao,” alisema Nyakiroto.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo na majeruhi wanaendelea na matibabu na hali zao zitapoonekana kuimarika wataruhusiwa.
No comments:
Post a Comment