Mamlaka ya reli ya
Tanzania na Zambia TAZARA imepokea injini nne mpya za umeme zinazotumia
mafuta ya dizeli pamoja na mabehewa 18 ya abiria yote kwa thamani ya
dola milioni 22.4.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania vifaa hivyo
vipya vilinunuliwa kupitia mkopo wa ushirikiano wa kiuchumi uliotiwa
sahihi na mataifa matatu ya Uchina ,Tanzania na Zambia mnamo tarehe 26
mwezi Machi mwaka 2012 mjini Lusaka.
Kulingana na taarifa
iliotolewa na TAZARA ,vifaa hivyo vipya vinalenga kuleta kuimarisha
pakubwa oparesheni za TAZARA,ambayo imekuwa ikizorota kutokana na vifaa
vilivyozeeka kutokana na ukosefu wa urekebishaji na fedha.
Ujio wa injini hizo nne utaongeza uwepo wa treni kila siku kwa asilimia 33 kutoka asilimia 12 na 1 Zikiwa zimezeeka kwa kati ya miaka 25 hadi 30,treni
nyingi zinazofanya kazi zimepita wakati wake na zimekuwa zikikumbwa na
hitilafu mara kwa mara,hali ambayo imesababishwa na kushindwa kwa
mamlaka kuzirekebisha kutokana na changamoto za kifedha.Akishuhudia
kupakuliwa kwa shehena ya vifaa hivyo katika bandari ya Dar es
Salaam,mkurugenzi wa TAZARA, Ronald Phiri alisema,''Tunaishukuru
serikali ya Uchina kwa ushirikiano wao mwema na TAZARA,ambayo ilisaidia
katika ujenzi wake miaka 40 iliopita''.
No comments:
Post a Comment