Jumamosi Novemba 21
Watford 1 Man United 2
Chelsea 1 Norwich 0
Everton 4 Aston Villa 0
Newcastle 0 Leicester 3
Southampton 0 Stoke 1
Swansea 2 Bournemouth 2
West Brom 2 Arsenal 1
2030 Man City v Liverpool
Bao za Jamie Vardy, Leonardo Ulloa na Okazaki zimewapa Leicester City ushindi wa 3-0 walipocheza Ugenini huko Saint James Park na Newcastle na kuwapaisha hadi kileleni mwa Ligi Kuu England ambako wanaweza kubaki ikiwa baadae Leo Man City hawatashinda Mechiyao na Liverpool.
Bao la Leo la Jamie Vardy limemfanya afikishe Bao 10 mfululizo kwenye Ligi na kumafanya aishike Rekodi ya Straika wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy aliefanya hivyo hapo hapo Saint James Park Mwaka 2003.
Ndani ya The Hawthorns, Arsenal walikwaa kisiki walipotunguliwa 2-1 na West Bromwich Albion waliotoka nyuma na kushinda Mechi hii ambayo Cazorla alikosa Penati ambayo ingewapa Sare.
Arsenal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya28 la Olivier Giroud na WBA kusawazisha kwa Bao la Dakika ya 35 la Morrison na kisha kujifunga mwenyewe kupitia Mikel Arteta katika Dakika ya 40 na kuwapa uongozi wa 2-1 WBA.
Arsenal walipata Penati katika Dakika ya 82 baada ya Chris Brunt kumchezea Faulo Alexis Sanchez lakini Santi Cazorla akapaisha.
Huko Stamford Bridge, Chelsea walimaliza uteja wa kuchapwa Mechi 3 mfululizo za Ligi kwa kuifunga Norwich City 1-0 kwa Bao la Dakika ya 64 la Diego Costa aliemalizia Frikiki ya Cesc Fabregas.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 22
1900 Tottenham v West Ham
Jumatatu Novemba 23
2300 Crystal Palace v Sunderland
No comments:
Post a Comment