SHEIKH ISSA PONDA |
MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Mkoa wa Morogoro, kwa mara nyingine tena imeahirisha hukumu ya
kesi ya jinai inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.
Kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu
yake leo Jumatano na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo
imeahirishwa na mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya hakimu husika
kutokuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa amekwenda kwenye kozi fupi ya
kushughulikia kesi za uchaguzi mjini Dodoma ambapo shauri hilo
limelazimika kuahirishwa na Hakimu Mkazi, Erick Rwehumbiza hadi Novemba
30, mwaka huu itakapofikishwa tena mahakamani hapo.
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka
mawili ikiwemo kutoa maneno yenye kuhimiza imani za dini na kushawishi
watu kutenda kosa, mashtaka anayodaiwa kuyatenda Agosti 2013.
Upande wa mashtaka wa kesi hiyo
unawakilishwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, Sunday
Hyera na George Mbalasa, wakati upande wa Mshitakiwa unawakilishwa na
Wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim na Bartholomeo Tarimo.
Awali hukumu ya Sheikh Ponda ilipangwa
kutolewa 19, 10 kabla ya kuahirishwa tena na shauri hilo kupangwa
kutolewa hukumu Novemba 18 mwaka huu, kabla ya kuahirishwa tena hii leo
hadi Novemba 30.
No comments:
Post a Comment