Tuesday, 2 August 2016

KAULI YA KWANZA YA SANE BAADA YA KUTUA MAN CITY

Leroy

Manchester City wamekamilisha usajili wa winga kutoka Schalke o4 Leroy Sane kwa mkataba wa miaka mitano.

Kinda huyo (20), ambaye alikuwa akiwaniwa na vilabu kadhaa barani Ulaya inaarifiwa amesajiliwa kwa ada ya paundi mil 37
Lakini inaelezwa kwamba, kiasi hicho cha pesa kinaweza kuongezeka mpaka paundi mil 42 endapo kijana  huyo atafanya vyema.
Sane, ambaye amekulia katika academy ya Schalke, amefunga magoli 13 kwenye michezo 57 aliyocheza na alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshiriki Michuano ya Euro mwaka huu.
“Najisikia faraja sana, nina furaha kuwa hapa. Sasa naweza kudumu hapa Manchester na kuichezea kwa mafanikio kilabu yangu,”amesema
“Moja ya sababu zilizonivutia kuja hala ni uwepo wa Pep Guardiola; alinishawsihi kuja hapa na kwamba ninaweza kuendeleza kipaji changu zaidi. Najua nitajifunza mambo mengi kutoka kwake na namna ambavyo nitendeleza kipaji chagu zaidi.”
“Nilimfuatilia kwa ukaribu Pep wakati yuko Barcelona na Bayern ambapo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa na alifanya kazi kubwa sana akiwa na wachezaji vijana.
“Nadhani anaweza kunifanya kuwa mchezaji niliyekamilika. Nadhani nitahitaji muda kidogo kuzoea kwasababu hii ni ligi nyingine na kuna aina tofauti ya uchezaji lakini nafikiri naweza kuzoea tu kwa haraka.”
Sane anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Guardiola kwenye dirisha hili la usajili, kufuatia ujio wa Ilkay Gundogan, Nolito, Oleksandr Zinchenko na  Aaron Mooy.
“Ana kipaji cha aina yake, ni mchezaji ambaye nafikiri mashabiki wetu watafuahi sana kumuangalia,” amesema Pep
“Ana uwezo mkubwa sana kiufundi, anajiamini akiwa na mpira, na kuna mengi ya kutamani kwa namna anavvyocheza mpira. Ana kasi, anatengeneza nafasi kwa wenzake, anajituma kwa ajili ya timu na vile vile anafunga. Pia mara zote amekuwa na mtazamo chanya na kwa hakika atafiti vizuri kwenye mfumo wetu.
Kwa umri wake wa miaka 20, bado ana mengi ya kujifunza lakini pia yuko kwenye kikosi cha timu ya taifa na nadhani atakuwa ni hazina kubwa ya klabu. Tuna furaha kubwa kuona ameungana nasi.

No comments:

Post a Comment